DUNIANI kuna vituko! ‘Blauzi’ ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’ imezua gumzo la aina yake.
Gumzo hilo lilizuka hivi karibuni katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram ikiwa ni baada ya wikiendi iliyopita mwanamuziki huyo kutinga ‘blauzi’ hiyo kwenye Tamasha la Fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
“Duu kweli msanii anavaa naiti dress sijui ndo zile za…. kamuwachia ukumbusho, makubwa ya Mungu mengi,” aliandika Ashakhamisi6 chini ya picha ya Kiba aliyokuwa amevaa ‘blauzi hiyo’ ambayo iliwekwa na watu mbalimbali kwenye kurasa zao za Instagram.