MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve’ amewataka mastaa kuacha unafiki wa kuposti watu mitandaoni baada ya kufariki dunia huku kwenye misiba wakiwa hawaudhurii.
Akichezesha taya na Amani, Steve alisema wasanii wamekuwa wanafiki, wanapenda kuonekena wema mbele za watu, yaani mashabiki zao kwenye mitandao ya kijamii, lakini inapofika siku ya kuzika, kila mtu anajichimbia, hawaonekani kama ilivyokuwa kwenye msiba wa msanii mwenzao, Seth Bosco aliyefariki dunia hivi karibuni.
“Mastaa ni wanafiki sana, eti wanaposti mtu akifa, lakini siyo washughulikaji kwenye msiba, mimi huo narudia tena ni unafiki mkubwa,” alisema Steve.
Stori: Imelda Mtema