×

Vijana Wanaokula Paka… ‘Wanakula Hadi Nyama za Watu’

EEEH bwana eee; upepo wa vijana Stanslaus Luchano ‘Ghost’ (23) na Nicholas Michael ‘Chaupepo’ (28) wakazi wa Kimara jijini Dar es Salaam waliochinja, kula nyama mbichi ya paka hivi karibuni umegeuka, sasa wamedaiwa kula nyama za watu; Amani linakupakulia ishu nzima.

 

Vijana hao wametuhumiwa na baadhi ya watu kuwa wanakula nyama za watu baada ya tukio lao la kula paka lililoripotiwa na vyombo vya habari vya Global kuendelea mitandaoni.

Global TV Online Desemba 4 mwaka huu uliweka video ikionesha vijana hao wakichinja paka na kisha baadaye kula nyama yake mbichi kwa ugali huku Gazeti la Amani la wiki iliyopita likiandika tukio hilo kwa kina.

 

WALIVYOTUHUMIWA KULA NYAMA ZA WATU

Awali vijana hao waliona kama ni kitu cha kawaida, lakini mapokeo ya watu wengi waliofuatilia habari hiyo waliona si jambo la kawaida na hivyo kuwahusisha na ulaji wa nyama za watu.

“Hawa si bure, lazima watakuwa wanakula na nyama za watu naomba wachunguzwe,” mchangiaji mmoja kwenye mtandao wa Global TV aliandika komenti yake chini ya habari ya tukio lao.

 

Mwingine aliandika: “Watakuwa wanakula na watoto wetu hawa.” Komenti zenye maneno ya namna hii zilionekana kwenye mitandao kwa wingi.

Hata hivyo, haikujulikana baadaye nani alichukulia siriaz tukio hilo na kuwataarifu polisi.

 

VIJANA WAKAMATWA

Wakati mambo yakiendelea kuwa ‘hoti’ kwenye mitandao ya kijamii kuhusu vijana hao, mmoja kati yao alimwandikia mwandishi wetu ujumbe akimtaarifu kuwa wametiwa mbaroni.

 

“Tumekamatwa tukihusishwa na ulaji nyama za watu, tunapelekwa polisi.” Ujumbe ulisomeka.

Baadaye mwandishi wetu alipojaribu kuwapigia ili kujua kilichowasibu vijana hao, hawakupatikana kutokana na simu zao kutopokelewa.

Hata hivyo, habari za kukamatwa kwao ziliendelea kuthibitishwa na baadhi ya majirani.

 

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu ili kuthibitisha kukamatwa kwa vijana hao kuhusiana na kutuhumiwa kula nyama za watu alisema:

“Niko kwenye kikao nipigie baadaye.”

Alipotafutwa baadaye simu yake iliita bila kupokelewa.

 

HABARI YAO YAZIDI KUWA GUMZO

Hata hivyo, habari ya vijana hao kuchinja na kula nyama za watu imezidi kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo kwa Global Tv watu zaidi ya 28, 000 wameifuatilia.

Kwenye mitandao mingine ya kijamii tukio lao halijapoa hata kidogo, gumzo na komenti za ujumbe tofautofauti zipo kama zote.

 

ONJA MAHOJIANO KATI YA VIJANA HAO NA GAZETI LA AMANI

Wiki iliyopita Amani lilianza kufanya mahojiano na vijana hao baada ya kupata tukio lao hilo la ajabu ambapo kwa kuanza lilimuliza Ghost:

 

Amani: Hebu tupe kwanza historia yako kwa ufupi?

Ghost: Mimi tangu nikiwa mdogo nimelelewa na bibi yangu baada ya mama yangu kufariki dunia na baba yangu kunitelekeza, wakati nakua nikawa namuona bibi anakula ngedere wale wanaokula mahindi na vitu vingine vingi vya ajabuajabu lakini akivipika.

 

Kuna kipindi nilikuwa naogopa lakini baadaye nikaja kuzoea ile hali. Ilifika wakati nikawa naenda mtoni na mimi kuvua samaki ambao kuna muda nikawa nawakuta wamekaa pamoja na vyura, nikawa nakula tu vibichi.

 

Amani: Mara ya kwanza unaanza kuishi na watu wengine tofauti haukupata shida wakati wa kula vyama mbichi?

Ghost: Nilichokuwa nakifanya ikifika jioni naondoka naenda mtaani kutafuta chakula kama paka, kenge, mbwa, minyoo nk kisha nakula hukohuko.

 

Kwa upande wake Chaupepo ambaye ni rafiki wa Ghost mahojiano yake kwa ufupi alisema:

“Mimi ni dereva bodaboda, nilikutana na Ghost, akanipa wazo hili la kuwa tunakula vitu vya ajabu, awali nilikuwa mzito kidogo lakini baadaye niliridhia.

“Nilikubali sababu niliona tunaweza kujiongezea pia kipato kutokana na kuitwa na watu mbalimbali katika matamasha yao,” alisema.

 

Chaupepo ameoa mke aitwaye Pendo ambaye aliliambia Amani Mtandaoni kuwa haoni cha ajabu chochote kwa mumewe kula nyama za paka mbichi.

“Mimi napika tu ugali, mboga yake mbichi anaitengeneza mwenyewe sioni ubaya,” alisema Pendo.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani

 

Mshtuko Dar! Vijana Wachinja, Wala Nyama Mbichi ya Paka

 

Leave a Comment