×

Zama Avunja Ukimya Kuajiriwa na Harmonize

KUFUATIA kuzagaa kwa taarifa mitandaoni kuwa, runinga aliyoizindua hivi karibuni siyo yake, bali ni mali ya staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize, mtangazaji Zamaradi Mketema ‘Zama’ amevunja ukimya kuwa, kwa sasa hawezi kuajiriwa.

Zama ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa, anashangaa ni kwa nini watu wanasema hivyo au labda ni kwa sababu Harmonize au Harmo ndiye mtu wa kwanza kuhojiwa kwenye runinga hiyo.

 

“Kwa hapa nilipofikia, siwezi kuajiriwa. Harmonize aniajiri mimi? Haiwezekani, nimejiajiri mwenyewe,” amesema Zama.

Stori: Imelda Mtema, Dar

 

Leave a Comment