
MWANADASHOSTI wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper, amevunja ukimya juu ya penzi lake na msanii wa Bongo Fleva, Eric Msodoki ‘Young Killer’.
Kwa muda mrefu, kumekuwa na madai mtandaoni kuwa, wawili hao ni mtu na mtuwe. Akizungumza na Over Ze Weekend, Wolper amesema, hakuna mapenzi kati yao, bali wanafanya tamthiliya.
“Mambo ya kunadi uhusiano wangu mitandaoni niliachana nayo miaka minne iliyopita kwa sababu kwangu hayana maana kabisa na hata mambo ya Young Killer kama angekuwa mpenzi wangu, nisingekubali kumuweka,” amesema Wolper.
STORI: IMELDA MTEMA