×

Timu Ya Bunge Ilivyofanya Mazoezi Nchini Uganda

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba na Mhe Cosato Chumi wakifanya mazoezi ya mwisho chini ya kocha Mhe Mwamoto akisaidiwa na Mhe Ally Ngali nchini Uganda.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ambaye anachezea timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazoezi ya kupiga mpira.
Picha ya pamoja ya Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Timu ya Bunge sport Club maarufu Ndugai Boys wakiwa katika mazoezi mepesi leo asubuhi kabla ya kukutana na timu mwenyeji Bunge la Uganda leo jioni katika Uwanja wa KCC Mjini Kampala Uganda.

 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mashariki ni miongoni mwa wachezaji wa Timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye mapema leo kabla ya mchezo wao alionekana akifanya mazoezi vilivyo ili kuweza kujipanga katika mechi hiyo.

 

Michezo hiyo inatarajiwa kumaliza leo jioni na timu ya Bunge na msafara mzima unatarajia kurudi nyumbani Tanzania siku ya ijumaa Desemba  20, 2019  ikiwa na matumaini ya ushindi na kujizolea medali nyingi katika michezo hiyo.

Leave a Comment