×

CEED Tanzania Yawapa Mbinu za Kisasa Wajasiriamali Moro

Victor Mfinanga ambaye ni Mkurugenzi wa Shambani Milk na mwanachama wa CEED akieleza umuhumi wa kuungana kama wajasiriamali.

 

KITUO cha Ujasiriamali cha CEED Tanzania, kimetoa mafunzo ya uendeshaji na usimamizi wa biashara kwa wajasiriamali mkoani Morogoro yenye lengo la kuwawezesha namna ya kusimamia biashara zao, kushirikiana pamoja katika kutatua changamoto za kibiashara pamoja na fursa mbalimbali mkoani humo.

 

Akizungumza na wajasiriamali wa mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa CEED Tanzania, Bw. Atiba Amalile, amewakumbusha wajasiriamali hao kuwa ‘’Haitakuwa biashahara kama kawaida ikiwa Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati miaka ijayo’’.

 

Naye mshauri wa Masuala ya Kodi na Mwakilishi wa CEED Tanzania jijini Dodoma, Bw. Baptist Mnyalape  amewahimiza wajasiriamali wa Morogoro kuhakikisha wanafahamu kanuni zinazoweza kuathiri biashara zao moja kwa moja.

 

Bw. Fred akieleza kuhusu CEED Tanzania.

 

‘’Nahitaji kuwakumbusha tu ndugu zangu wajasiriamali kuhusu kuzingatia masuala ya kodi, tuhakikishe tunafahamu kanuni na sheria ambazo zinaweza kuingilia na kuathiri biashara zetu moja kwa moja, ukishindwa kuzingatia haya itagharimu muda wako pamoja na pesa zako,’ alisema Mnyalape.

 

Kwa upande wa Mwakilishi kutoka CRDB Benki, Dennis Kayanda amewasisitizia wajasiriamali hao juu ya umuhimu wa kufuata sheria ya matumizi ya ushuru wa ardhi na kusema; “Ni hatari zaidi kwa kutafuta mikopo kutoka benki za biashara na kuwekeza katika biashara ambazo zinaweza kuwa hazifanyi kazi katika eneo hilo na hivyo kuathiri biashara”.

 

Aidha, mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo na Mkurugenzi Mtendaji wa Maziwa Shambani Milk mkoani Morogoro, Victor Mfinanga amefurahia kupata nafasi tena kwani mafunzo haya yannamuwezesha kufahamu namna ya kuendesha biashara yake.

 

Baadhi ya wajasiriamali wakijatambulisha na kuongea kuhusu biashara zao.

 

‘‘Nimekuwa nikihudhuria mara kwa mara mafunzo ya CEED, mfano mafunzo yaliyokuwa yakitolewa jijini Dar es Salaam na CEED Tanzania yamenisaida kujua habari za biashara bora, namna ambavyo mtu unawezakutumia teknolojia kujifunza namna ya kuendesha biashara yako,’’ alisema Mfinanga.

 

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wajasiriamali mbalimbali wa mkoani Morogoro, bila kusahau
wawakilishi kutoka benki za CRDB, NMB NBC, Azania, pamoja na Benki ya Afrika ambazo kwa pamoja zimewapa elimu wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo bila shida na namna ya kutumia mikopo hiyo kukuza biashara zao.

 

Vile vile Chama Cha Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania mkoani Morogoro kilipata nafasi ya kushiriki mafunzo haya jinsi ya kukuza na kujenga biashara za ushindani sokoni.

 

‘UA’ LINALOFUTA DHAMBI: WASANII WAKIMBIZANA KUTUBU, ONA HAPA

Leave a Comment