×

Kauli 10 za Kwanza Za Arteta

 

MIKEL Arteta ameanza maisha yake ya kwanza akiwa kocha mkuu. Ameteuliwa kuinoa Arsenal akitoka kuwa msaidizi wa Pep Guardiola katika kikosi cha Manchester City.

 

Arteta, 37, inaelezwa amepelekwa Arsenal ili kurudisha utamaduni wao wa soka la kuvutia la pasi nyingi na kushambulia ambalo lilipotea tangu alipoondoka mzee Arsene Wenger. Mara baada ya kukanyaga Emirates, Arteta kazungumza kauli kumi muhimu katika kuleta mabadiliko klabuni hapo.

 

1) USHAWISHI

“Natakiwa kujaribu kuwashawishi wachezaji kuhusu nini nataka kufanya, nikifanye kwa jinsi gani, wanatakiwa kuanza kukubali mchakato mpya, njia tofauti ya kufi kiri. Nataka kila mtumishi na kila mmoja katika klabu tuwe na fi kira moja. Tunatakiwa kujenga utamaduni ambao utatubeba wote.”

 

2) SOKA LA KUVUTIA

“Nataka timu iwe inamiliki mpira, inayocheza kwa kasi, wapinzani wacheze muda wote kwenye eneo lao.”

 

3) KUANZA KUSHINDA HARAKA

“Hatuna pre-season. Tunatakiwa kujikita katika mambo ambayo yatakuwa na faida haraka, katika muda mfupi. Hatujajadili kuhusu dirisha la usajili. Ninachokitaka ni kujaribu kushinda mechi sasa na kutafuta mbinu ya kuboresha kiwango ili kuleta hali ya kujiamini ili waingie uwanjani wakiwa vizuri zaidi ya walivyokuwa.”

 

4) KUHESHIMIANA

“Tunatakiwa kujiwekea kanuni za kuishi, kuwasiliana, kuheshimiana. Masuala ya heshima ni lazima yazingatiwe. Wakiyafuata watacheza hapa. Wasipofuata, wataondoka.”

 

5) UKALI

“Nilichojifunza zaidi kwa Pep Guardiola ni kwamba unatakiwa kuwa mkali na unatakiwa kupambana kila siku kutengeneza roho za ushindi. Nataka watu wawajibike katika kazi zao na watu ambao wanajitoa kwa nguvu na kwa moyo. Yeyote ambaye hatafuata haya au ambaye atakuwa na madhara hasi, hatafaa katika mazingira haya au utamaduni huu.”

 

6) KUWAELEWA WACHEZAJI

“Nahitaji kuwaelewa wachezaji, namna gani wanafi kiri na kitu gani wanakikosa. Kama nikifi kia hatua hiyo, naweza kuwasaidia waniamini na wanifuate.

 

7) MATAJI

“Hii ni heshima kubwa. soka na hilo limewekwa wazi vizuri kabisa kwangu katika mazungumzo yangu na Stan na Josh Kroenke, na watu wakubwa klabuni. Sote tunajua kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufi kia lengo hilo lakini nina uhakika tutafanikiwa.”

 

8) HAKUNA PAPARA

“Ninajua vizuri kabisa kwamba mafanikio hayatakuja haraka lakini kikosi cha sasa kina vipaji vya kutosha na kuna utitiri wa vijana wenye vipaji wanaotokea kwenye akademi.”

 

9) KUWASHAWISHI LACAZETTE, AUBAMEYANG KUBAKI

“Hicho ndiyo kitu ambacho tumekuwa tukikizungumza. Kama tunaweza kutengeneza utamaduni ambao kila mmoja anawajibika, tunaweza kuleta uongozi kwenye timu na matarajio na kujitoa na muelekeo unaoonekana na halafu tutatengeneza utambulisho. Kama wachezaji wakijisikia ni sehemu ya utambulisho huo, watataka kubaki kwa sababu wataufurahia.

 

“Kwa sasa nahisi kama vile wachezaji hao wanateseka. Unapoteseka, wakati mwingine unaweza kutaka kuondoka. Unapofurahia unataka kuwa sehemu ya kitu.”

 

10) HAWEKI MALENGO

“Kuweka malengo ni kitu ambacho sikitaki. Malengo ya klabu hii yapo wazi. Unatakiwa upambanie makombe na kuwa kwenye Ligi ya Mabingwa.

 

“Kipaumbele cha kwanza ni kubadili nguvu. Nataka kila mmoja katika klabu hii tuwaze kitu kimoja. Nitajitolea kila tone la damu kwa ajili ya klabu hii iwe bora.”

 

LONDON, England

Leave a Comment