×

Mkwasa: Tutawafunga Simba Bila Shida

 

 

Kocha wa muda wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa.

KOCHA wa muda wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anaamini watawafunga Simba katika mchezo wa Januari nne, mwakani kwa kuwa safu yake ya ushambuliaji imeshaanza kupika mabao.

 

Mkwasa amesema tatizo kubwa ambalo lilikuwa linaisumbua timu yake ni kushindwa kutengeneza nafasi za mabao, jambo ambalo amelifanyia kazi na limeanza kuzaa matunda.

Yanga walipata ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa FA waliocheza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Jumamosi iliyopita dhidi ya Iringa United kisha wakasuluhu dhidi ya Mbeya City huku Uwanja wa Sokine ukiwa siyo rafiki kutokana na mvua kubwa iliyonyesha uwanjani hapo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mkwasa alisema Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu nyingine, kwa kuwa shida kubwa ambayo ilikuwa inaisumbua klabu hiyo ni kushindwa kufunga mabao jambo ambalo wamelifanyia kazi na watapata mabao katika kila mchezo, ukiwemo huo wa Simba.

 

“Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu nyingine, tulikuwa na tatizo la kushindwa kupata mabao kwenye safu yetu ya ushambuliaji, tatizo ambalo kwa sasa limepatiwa ufumbuzi, kwa hiyo lengo letu ni kushinda katika kila mchezo hadi huo wa Januari nne,” alisema Mkwasa.

Na Mwandishi Wetu

Leave a Comment