×

Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo Wakwea Pipa

Mshindi wa safari ya kwenda Mbuga za Wanyama za Serengeti wa Ibuka kidedea na NBC Malengo, Esther Ndunguru (kushoto) akikaguliwa tiketi yake kabla ya kupanda ndege.
Meneja Masoko wa benki ya NBC,  Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi tiketi ya ndege ya kwa moja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Esther  Ndunguru muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakifungua shampeni muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo wakielekea Seychelles. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, kila mwezi washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki za miguu mitatu (Toyo).
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipozi kwa picha pamoja na  wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Huku wakiwa wameshika glasi zenye shampeni ikiwa ni ishara ya kuwatakia safari njema.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakipozi kwa picha pamoja na  wawakilishi wa NBC waliowasindikiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakiwa katika hatua ya mwisho ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaa.
Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza wa Benki ya NBC, Dorothea Mabonye (kushoto), pamoja na Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), wakiagana na mmoja wa washindi wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Ramdhani Saidi (kulia) muda mfupi kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Ambapo alikuwa akielekea Seychelles pamoja na mwenza wake. Kupitia kampeni hiyo inayoendelea, washindi wanajishindia safari za kitalii kwenda Seychelles, mbuga za wanyama za Serengeti, bodaboda na pikipiki ya miguu mitatu (Toyo).

Leave a Comment