×

Mkesha Maalum na wa Kipekee wa Kufunga Mwaka 2019

 

Shalom Tanzania! Kwa mara nyingine tena, Kanisa la Christ Mandate and Power Ministries International linawaletea ibada ya mkesha wa kuvuka mwaka 2019 kuingia 2020 utakayofanyika katika Viwanja vya TFF Karume, Dar es Salaam, Desemba 31, 2019, kuanzia saa moja jioni hadi alfajiri ya tarehe 1 Januari 2020.

Mtumishi wa Yesu, Malachi Joseph anakukaribisha katika mkesha huu mkubwa wa kukutoa katika kiwango kimoja cha utukufu kwenda kingine.

Tarajia matendo makuu ya Mungu kupitia mkesha huu. Ni usiku ambao hautasahaulika kwa haraka. Ni usiku wa kuoshwa miguu na kuchukua hatua mpya za kuingia 2020 pamoja na Mungu. Ni usiku wa kuliombea taifa letu la Tanzania.

 

Ni usiku ambao sauti ya Mungu itajidhihirisha kupitia Mtumishi wa Yesu Malachi Joseph na kuharibu nguvu za giza zilizokufunga. Ni usiku ambao ulimwengu wa giza utaingia matatani.

Usikose siku hii ya kihistoria.
Tarajia miujiza ya Mungu, uponyaji na kufungiliwa. Walemavu watatembea, vipofu wataona na viziwi watasikia.

Njoo tumsifu na kumuabudu Mungu pamoja na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili ili neema ya Mungu ianze na wewe kwa mwaka mpya 2020; akiwemo Joel Lwaga, John Lissu, Cosmas Chidumule, Venance Malachi na wengine wengi.

Kwa maelezo zaidi piga namba: +255 765 219 203 au +255 766 925 848

 

 

 

Leave a Comment