×

Afariki kwa Kupigwa na Radi Akichuma Maembe

 

MWANAMKE mmoja mkazi wa Kata ya Ng’ambo Manispaa ya Tabora, Rehema Simende amefariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akichuma maembe wakati mvua ikinyesha katika eneo la Mtaa wa Mtakuja.

 

Kufuatia tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha Jeshi la Polisi wilaya ya Tabora limewasili katika eneo la tukio na kupokea taarifa kutoka kwa mashuuda wa tukio hilo akiwemo Babu wa marehemu Mzee Juma Shabani.

 

Aidha, Kamanda Mwakalukwa amewataka Wananchi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mbalimbali ya mkoani Tabora.

 

Jeshi la polisi mkoa wa Tabora limetoa wito kwa wakazi wote wa mkoa huu kusherehekea sikuku ya mwaka mpya kwa amani na utulivu.

 

Leave a Comment