
YULE golikipa wa kimataifa wa Zambia, Toaster Nsabata, anatarajiwa kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza taratibu za usajili ndani ya Simba ikiwa ni pamoja na kufanyiwa majaribio kwa kipindi cha wiki moja.
Nsabata ambaye ana miaka 30, kwa sasa ni nahodha wa Zanaco FC ambayo anaitumikia tangu alipojiunga nayo mwaka 2015.
Chanzo kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Spoti Xtra, kuwa: “Viongozi wa Simba kwa sasa wanahangaika jinsi ya kuhakisha kipa huyo anatua hapa nchini kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo.

“Nadhani kipa huyo anajiamini kutokana na uwezo wake kuwa wa hali ya juu ndio maana amekubali kufanyiwa hayo majaribio akiwa na imani kuwa atafanikiwa.
”Nsabata licha ya kukitumikia kikosi cha Zanaco kwa mafanikio makubwa, pia kipa huyo ni moja kati ya makipa wakubwa nchini Zambia kwani amekitumikia kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa.
STORI NA MARCO MZUMBE NA MUSSA MATEJA,