×

Linah Hawezi Kubadili Dini, Kisa Ndoa

MWANAMAMA anayefanya poa kunako Bongo Fleva, Estarlina Sanga ‘Linah’ ni mmoja wa mastaa wa kike ambao hawawezi kubadili dini kwa sababu ya mapenzi.

 

Linah ambaye ni Mkristo aliliambia IJUMAA WIKIENDA kuwa pamoja na baba mtoto wake kuwa Muislam, lakini suala la kubadili dini ili kuivuta ndoa ni gumu kwake.

 

“Unajua kiimani hutakiwa kufanya vitu juujuu, hata ukibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu siyo kwa sababu ya mapenzi, kwa hiyo mimi sikutaka kufanya hiyo michezo,” amesema Linah.

 

Pengine Linah aliona mbali kwani mpaka sasa hayupo tena kwenye uhusiano na baba mtoto wake na anatajwa kutoka kimapenzi na DJ wa staa wa Bongo Fleva, DJ Seven.

STORI: NEEMA ADRIAN, DAR

Leave a Comment