×

Mkwasa, Kahata Watwaa Tuzo ya Mwezi Desemba Ligi Kuu Bara

Kaimu Kocha wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ametangazwa kuwa kocha bora kwa mwezi uliopita.
Mkwasa ametwaa tuzo ya ukocha bora ikiwa ni muda mchache tangu achukue nafasi hiyo Yanga baada ya kuondoka kwa Mwinyi Zahera ambaye alikuwa anaiona timu hiyo.

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Francis Kahata amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Disemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/20, akiwashinda Hassan Dilunga wa Simba na Bakari Mwanyeto wa Coastal Union alioingia nao fainali.

Leave a Comment