×

Cameroon: Bomu Laua 9 na Kujeruhi 30

MLIPUKO katika mji wa Fotokol mpakani mwa Cameroon na Nigeria umesababisha vifo vya watu tisa na kujeruhi wengine 30.

 

Gavana wa eneo hilo Midjiyawa Bakari amesema mlipuko huo umetokea baada ya kijana mmoja kuchukua kifaa cha kulipuka akidhani ni kipande cha chuma. Kijana huyo pamoja na watu wengine nane wamepoteza maisha.

 

Tayari Maafisa wanafanya uchunguzi kufahamu chimbuko la kifaa hicho lakini inadhaniwa kuwa kinatoka kwa Wanajeshi wanaopigana na Boko Haram au kwa Boko Haram wenyewe.

 

Maafisa hao wametoa tahadhari juu ya uwepo wa mabomu ya ardhini na silaha ambazo zimetelekezwa au kupotea.

 

Mapigano ya Boko Haram yalianzia nchini Nigeria takriban miaka 10 iliyopita lakini hivi sasa yamevuka mipaka na kuingia nchi jirani za Cameroon, Niger na Chad.

 

Leave a Comment