
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Dkt Augustine Mrema amemwandikia barua Mhe. Rais John Pombe Magufuli kumuomba serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imulipe Sh.Bilioni 2 kwa kumbambikizia kesi namba 2 ya mwaka 1997 ya kumuhusisha Rais Benjamini Mkapa na rushwa ya sh Milioni 500, ikiwa na lengo la kummaliza kisiasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mrema amesema ameona afikishe kilio chake cha muda mrefu kwa Rais wa wanyonge,kuhusu mambo mabaya aliyofanyiwa ya kukamatwa na kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa lengo la kumuondoa kwenye ulingo wa kisiasa kwa kumtupa gerezani.
“Iliundwa kamati ya bunge kuchunguza nyaraka zilizokuwa zikihusisha tuhuma za rushwa dhidi ya vigogo mbalimbali baada ya kamati hiyo kufanya uchunguzi ililidhia kuwa sikuwa na hatia nikapewa cheti Cha kinga,” amesema Mrema.