
Januari 3, 2020, tukio lisilo la kawaida lilitokea nchini Iraq, likimhusisha kiongozi wa ngazi za juu wa jeshi la Iran! Huyu si mwingine bali ni Qasem Soleimani, Jenerali wa kikosi maalum cha Qudsi ambaye aliuawa katika shambulizi la jeshi la Marekani jijini Baghdad.
Muda mfupi baada ya kifo chake, dunia ni kama ilitingishika na mpaka sasa hali si shwari! Bei ya mafuta ilipanda kwa kasi kufuatia kifo cha Qasem, Iran ikatishia kulipa kisasi kwa Marekani, Marekani nayo ikajigamba kwamba haiogopi chochote kwa sababu ni taifa lenye nguvu, hivyo kuzua hofu ya vita ya dunia.