
POLISI mkoani Kagera inamshikilia kijana mmoja, Alfred Kamugisha, mkazi wa Kijiji cha Kishaanda, Kata ya Kibale wilayani Kyerwa kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma mkuki askari wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kufanya vitendo vya ujangili ndani ya hifadhi mpya ya Rumanyika.