
WATU watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na Somalia.
Walimu watatu ambao si wa eneo hilo waliuawa kwa kupigwa risasi huku kituo kimoja cha Polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.
Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka. Polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama zikionyoesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika barabara ya eneo hilo
Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.
Hili ni shambulizi ya 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya katika kipindi cha wiki sita ambapo mashambulizi manne yamefanywa Garissa, matatu Wajir, mawili Mandera na mawili Lamu.