
ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ afanye shoo ya miaka 10 ya muziki wake nyumbani kwao, Kigoma, mzazi mwenza wa msanii Aslay, Tessy Abdul ‘Tessychocolate’ ameeleza kubadilishwa na msanii huyo.
Tessy ambaye alikuwa ni miongoni mwa waliokwenda Kigoma, aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa alifurahi mno kupata mwaliko huo na ilikuwa ni kama ‘suprise’ na walipofika Kigoma na Diamond au Mondi alimpandisha stejini kuzungumza chochote, jambo ambalo anaamini limemfungulia njia zaidi.
“Nilifurahi sana Diamond aliponiita jukwaani na kunipa nafasi ya kuongea, ilikuwa kama surprise kwangu kwa sababu ni kitu ambacho sijawahi kukifanya, namshukuru sana kwa sababu naamini sasa mambo yangu yataenda vizuri maana amenibadilisha na nimekuwa na ujasiri zaidi,” amesema Tessy.
Stori: Memorise Richard, Dar