×

Mwijaku Aibuka na Tausi Kuzaa Nje ya Ndoa “Kwani Hana Hisia?” – Video

MTANGAZAJI na msanii ambaye amejizolea umaarufu kwa kukosoa mahusiano ya wasanii wa Bongo, Mwijaku amevunja ukimya na kuwafungukia wote waliokuwa wakimsema vibaya msanii wa Bongo Movie na Comedian, Tausi Mdegela baada ya kujifungua hivi karibuni.

 

Akipiga stori kupitia exclusive interview na Global TV Online, Mwijaku amwetaka watu hao waliokuwa wakimsema vibaya Tausi kutokana na maumbile yake ya ufupi wakilinganisha na kujifungua kwake, watubu ili wawe salama.

 

“Kwani yeye siyo mwanamke, hana hisia, hafai kupendwa? Nilidhani watu wangehoji kwa nini amezaa kabla ya kuolewa lakini wanahoji eti huyu naye kazaa, walitakaje kumbe? Sisi sote tumeumbwa na mungu na ana makusudi yake kwa kila aliyemuumba. Mimi nawataka waliomsema vibaya Tausi watubu ili wawe salama,” amesema Mwijaku.

 

Leave a Comment