×

Official Lyyn: Ntafanya Kolabo na Tanasha – Video

Msanii wa Bongo Fleva na Video Vixen maarufu Bongo, Official Lyyn, leo Jumatatu, januari 20, 2020, amefanya Exclusive interview na +255 Global Radio na kuzungumzia mambo kadha ikiwemo mahusiano yake na Diamond kwa sasa baada ya kuachana na amedai kuwa kwa sasa yupo single (haba boyfriend) na kwamba anatamani sana kufanya Kolabo na Tanasha ambayo itakuwa habari nyingine mjini.

 

Lyyn ameanika simulizi ya maisha yake ya muziki kutoka kuwa video vixen mpaka mwanamuziki wa Bongo Fleva. Na kufungukia kuhusu changamoto anazopitia kwa wale wanaomuona hajui kuimba na jinsi anavyozikabili akiamini hakuna kama yeye kwani ni mwanamke mchapakazi, mzuri na anaejiamini.

Wimbo wake uliopo kwenye chati kwa sasa ni “Pepea” ulotoka miezi kadhaa iliyopita na kuahidi kutoa ngoma mbalimbali kwa mwaka 2020 ikiwemo Hola Hola na kuomba mashabiki zake wakae mkao wa kula.

 

Kuhusu mimba na mahusiano yake ya sasa na Diamond, Tazama video hii.

Leave a Comment