
Ripoti mpya ya kila mwaka ya kielelezo cha demokrasia iliyochapishwa na Kitengo cha Ujasusi wa Kiuchumi EIU imesema kiwango cha demokrasia Afrika kilishuka mwaka 2019 jambo linalotia wasiwasi wa kurudi nyuma kwa demokrasia katika sehemu nyingi duniani.
Shirika hilo limesema kiwango cha demokrasia kote duniani kilishuka kutoka 5.48 mwaka 2018 hadi 5.44 mwaka 2019.
Shirika hilo linaweka makadirio yake ya demokrasia kutokana na hoja tano, uhuru wa raia, utamaduni wa kisiasa, ushiriki wa raia katika masuala ya kisiasa, uongozi na mchakato wa uchaguzi, na limefanya uchunguzi huo katika nchi 165 kote duniani.
Mauritius ndiyo nchi ya pekee ya Afrika iliyotajwa kuwa na demokrasia kikamilifu huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa chini kabisa kwenye orodha ikidaiwa kuendeshwa kwa mfumo wa kidikteta.