×

Arsenal Yaanza Mazungumzo Kumnasa Lemar

ARSENAL imeripotiwa wapo kwenye mazungumzo na Atletico Madrid wakitaka kumsajili winga Thomas Lemar katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo la Januari.

 

Klabu hiyo tayari imeshafanya mazungumzo na nyota huyo pamoja na klabu yake ikitaka kumsajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa pande zote mbili bado hazijakaribia kwenye makubaliano. Lakini imeelezwa kuwa lolote linaweza kutokea kabla ya dirisha kufungwa.

 

Mfaransa huyo, 24, yupo katika msimu wake wa pili Atletico Madrid lakini ameshindwa kung’aa msimu huu akiwa hajafunga bao lolote katika mechi 21 alizocheza.

Tayari kocha wake Diego Simeone amekiri kwamba nyota huyo yupo chini ya kiwango na uvumilivu unaelekea kumshinda.

 

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anaamini ni wakati sahihi wa kumchukua Lemar akiamini ataweza kuwasaidia katika jitihada zao za kutafuta nafasi ndani ya nne bora.

LONDON, England

Leave a Comment