×

Global Radio Marekani: Tazama Helkopta Ilivyomuua Kobe Bryant – Video

KUFUATIA kifo cha mchezaji nguli wa mpira wa kikapu duniani aliyekuwa akikipiga kwenye Ligi ya NBA Marekani, Kobe Bryant (41), ambaye amefariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana huko mji wa Calabasas, California, Global TV Online na +255 Global Radio tupo eneo la tukio, nchini Marekani kukupasha habari kila kinachoendelea.

Katika ajali hiyo, Helikopta hiyo inadaiwa kuwa ilizunguka mara kadhaa angani kisha kuwaka moto kabla ya kuanguka na kuua watu wote watano akiwemo binti wa #KobeBryant, Gianna Maria Onore ‘Gigi’ (13).

TAZAMA RIPOTA WA GLOBAL TV NA GLOBA RADIO (MAREKANI) AKIELEZEA KUTOKA ENEO LA TUKKIO

 

Bryant, ambaye ni bingwa wa NBA mara tano,  alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora wa vikapu.

 

Bryant alikuwa nani?

Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa miaka 20 katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.

Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.

 

Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olimpiki. Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015. Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

 

Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wa kike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri. Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.

Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani. Ingawa baadaye aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

 

Watu wanasemaje kuhusu kifo cha nyota huyo?

Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufuatia taarifa ya ajali hiyo. Shaquille O’Neal, ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004, alisema hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo. “Ninakupenda na utakumbukwa,” aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.

 

Deron Williams, aliyekuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. alimuelezeaBryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.

Leave a Comment