Rais JPM: Unanunua Drone Kwani Inazima Moto? – Video
Global Publishers January 27, 2020 0 Comments
SHARE THIS:
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, leo Jumatatu, Januari 27, 2020, amewaapisha, George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mussa Azzan ‘Zungu’ kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.
Aidha, Rais Magufuli amewaapia Mhe. Maimuna Kibenga, Hussein Athuman na Prof. Kennedy Godfrey ambao ni mabalozi wapya aliyowateua hivi karibuni, Ikulu jijini Dar es Salaam. Mabalozi hao wataiwakilisha Tanzania katika vituo vya Geneva-Uswisi, Tokyo-Japan na New York-Umoja wa Mataifa.
Kuhusu hizo fedha, Makamu wa Rais wa #WorldBank alikuja hapa mwaka jana na walitoa pesa wakijua Tanzania tuna misimamo gani kuhusu elimu, kwa hiyo hao wengine ni wapiga kelele tu, wengine msiwajibu maana watu wa namna hiyo wapo tu Duniani.
Hili la mikataba na Kampuni, Waziri Simbachwene kalimalize, nakupa haya mafaili yote ukayosome uchukue hatua. Naibu Waziri Masauni anajua ingawa hajahusika sana alikuwa akipewa tu dokezo, sifahamu kwanini alikaa kimya angeweza kuniambia, ila Katibu Mkuu alihusika sana.
Ni kweli kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani ninakupeleka katika wizara ngumu, kwani imehusika katika mambo ya ‘Scandal’ nyingi na Mawaziri wote wamekuwa wakiambiwa warekebishe lakini sifahamu huwa kuna mdudu gani pale sasa nimeona nikupeleke wewe nenda kayasimamie.
Wizara ya Mambo ya Ndani sijui ina mdudu gani umekua ikihusishwa na skendo nyingi, na mara nyingi nimekuwa nikiwaambia Mawaziri lakini sijui kuna mapepo gani pale, na wewe asije akakuingia, tunaliingizia Taifa hasara kwa mambo yasiyo na tija na Mikataba ya ajabu.
Mama Tarishi umekuwa tarishi mzuri, tunajua ulikuwa umestaafu ila kwa utendaji wako hatuwezi kukuacha ukastaafu ndio maana tumekupeleka #Geneva. Nendeni mkatusemee vizuri. Yapo mengi ya ajabu ila ninyi nendeni mkaseme vizuri kuhusu Tanzania maana mnaijua.
Ameongea hapa Waziri kuhusu la elimu, nisingependa kuongelea hilo maana Makamu wa Rais wa #WorldBank alikuja hapa. Wanatoa pesa wakijua tuna misimamo gani na tunafanya nini. Wengine hawa ni wapiga kelele, msiwe mnawajibu maana watu hao hawaishi Duniani.
Waziri wa Mambo ya Ndani umezungumza vizuri hapa kuwa huna nyota hata moja, Vyombo vya Ulinzi na Usamala vina namna ya kuviendesha. Ndio maana Waziri Mwinyi amekaa sana Wizara ya Ulinzi. Anajua, hawezi kukaa mbele hapa akawatukana Bregedia hawa.
Katumie mbinu hizo hizo. Ndio maana unaona Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wanaripoti moja kwa moja kwa Rais. Ukishapima hizo inaweza sana kukusaidia namna ya kufanya kazi. Wewe ni Mwanasheria, ndio maana umelianza hapa nikaona IGP anatikisa kichwa.
Nafikiri IGP amefurahi sana maana muda mwingine alikuwa anakuja kwangu analalamika, nimeshaambiwa hawa niwatoe. Huku akisema Order haisemi hivyo. Nikamuambia nenda kawatowe. Lakini kiukweli muda mwingine si utaratibu. Tukifuata utaratibu itaturahisishia.
Waziri wa Mambo ya Ndani suala la Kampuni walisaini MoU nenda kalimalize. Tena nakupa mafaili hapa hapa ukasome, kalale nayo mbele huko. Nataka nikupe tu tahadhari, watendaji wako utakaowakuta wanajua hili. Naibu Waziri anajua, ingawa hakuhusishwa sana.
Naibu Waziri alikuwa anapewa madokezo, alipokuwa akiyapata haya naye akawa ananyamaza, angeweza hata kuja Serikalini akaeleza. Sifahamu kwanini alikaa kimya ila hakuhusika sana. Naibu Katibu Mkuu amehusika tangu mwanzo hadi mwisho. Kwenye Zimamoto wapo.
Hao wa Jeshi la Zimamoto wengine ndio walikuwaa wanaenda wanalipwa wakishakaa kwenye kikao. Wamelipwa Dola 500 ya siti, wamepewa Dola 300 ya safari, wanapewa Laptop. Sasa jiulize, umeingia kwenye mazungumzo na unayezungumza naye kwanini akupe Dola 800.
Hao Watendaji hawakuliona hilo. Mkataba ukasainiwa, wakapelekwa nje, wakalipiwa. Wakanunuliwa na laptops. Wanaenda kununua Drones. Sijui itatumika kuzima moto? Watengeneza Drones, Marekani na Australia yanaungua mashamba hawatumii Drones. Nimeumia sana.
Haya ndio yanatupeleka Taifa kwenye kesi za ajabu. Juzi Mwanasheria Mkuu ameenda kule London kila mara anaenda kwa kesi ya utapeli. Watu wamekodisha ndege kwamba ATCL imekodisha, ilipofika hapa haikufanya safari hata moja ikatakiwa iende check up.
Ndege hiyo haikutumika ila tunashtakiwa kwa kudaiwa Dola Milioni 40 na watu walisaini, wapo wanazunguka. Miktaba kama hii inaingizia Taifa hasara. Mkataba huu wa MoU, haukuletwa hata kwenye Cabinet. Waziri aliyekutangulia anaandika tu barua niidhinishe.
Tusiingie kwenye mikataba bila kuihusisha Wizara inayohusika na kukopa pesa, tusiwaumize watanzania maskini kwa kwenda kusaini mikataba ya hovyo isiyo na maslahi kwa taifa. – Rais Magufuli.