Jeshi la Marekani limekiri kuanguka kwa ndege ya kijeshi chapa E-11A katika eneo la Ghazni nchini Afghanistan, huku likipinga madai yaliyotolewa na wanamgambo wa Taliban kwamba waliidungua ndege hiyo.
Msemaji wa Jeshi la Marekani kanali Sonny Legget amesema kwenye taarifa yake kwamba ingawa bado kunafanyika uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo, lakini hakuna dalili inayoashiria kwamba ilidunguliwa.

Maafisa waandamizi wa Afghanistan waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mamlaka ziliwafukuza watumishi wa eneo hilo kwenda kuyatambua mabaki ya ndege hiyo, katika eneo la milima ilikoanguka, ambako kwa sehemu kunadhibitiwa na Taliban.
Ndege hiyo ilianguka january 27 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wasiozidi kumi waliokuwemo ndani ya hiyo.
Ajali hiyo inakuja wakati Talibani na Marekani wakiwa kwenye mazungumzo ya kumaliza vita vilivyodumu kwa miaka 18 nchini Afghanistan.