×

Betika Latua kwa Wafanyabiashara wa Mabati & Mbao Buguruni

MAPEMA leo Jumatano, Oktoba 29, timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea wafanyabiashara wa mabati eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam na maeneo mengine ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulinadi zaidi.

Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo hayo wamesema kuwa wamefurahishwa na timu ya maofisa hao kufika eneo hilo kwani wamekuwa wakiona picha za wafanyabiashara wengine hivyo nao ni furaha yao nao kupiga picha wakiwa katika biashara zao.

Betika hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

 

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kwa kuwa mkombozi wao kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

 

 

 

Leave a Comment