
MTOTO mdogo aitwaye Baraka Shigongo (10) mwenye kipaji cha aina yake katika masuala mbalimbali hasa ya Sayansi, ameamua kuingia darasani kuchambua kitu kimoja baada ya kingine akiielezea jamii kuhusu homa hatari duniani ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.
Virusi vya Corona ambavyo vimeripotiwa vimesambaa nchini China na baadhi ya ameneo ya Bara la Asia na Marekani, mpaka sasa vimeua watu wapatao 132 na wengine bado wanaendelea kutibiwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Shirika la Afya Duniani linafanya jitihada za haraka na madhubuti ya kupambana na ugonjwa huo unaohofiwa kufika mpaka Bara la Afrika huku Serikali ya Tanzania nayo ikiwatahadharisha wananchi wake kuhusu ugonjwa huo licha ya kwamba haujafika nchini.
Kupitia YouTube channel yake, mtoto Baraka anaelezea ugonjwa huo ni nini, namna unavyoambukizwa na njia za kitaalam za kujikinga na Corona Virus.