×

Bunge la Ulaya Lapitisha Uingereza Kujitoa EU

WABUNGE wa bunge la Umoja wa Ulaya (EU) wamepitisha kwa wingi sheria inayoruhusu Uingereza kuondoka kwenye umoja huo, maarufu kama Brexit.

 

Bunge hilo limepiga kura ya kuyapitisha makubaliano ya Brexit kwa kura 621 dhidi ya 49 ambazo zilipinga mchakato huo kuendelea.

 

Nchi wanachama hivi sasa wanatakiwa kutoa idhini ya mwisho kwenye makubaliano hayo kupitia utaratibu wa maandishi.

 

Katika kipindi cha mchakato huo Uingereza itatakiwa kuendelea kutii masharti na sheria za umoja huo.

 

Uingereza inatarajiwa kuondoka katika umoja huo  usiku wa kuamkia Januari 31, 2020, baada ya miaka mitatu tangu Waingereza walipoanzisha mchakato wa kuondoka ama kusalia kwenye umoja huo katika kura ya maoni ya mwaka 2016.

Leave a Comment