
SHIRIKA la ndege la Kenya limesitisha safari zote za kwenda China baada ya mlipuko wa virusi vya corona.
Visa sita vya maambukizi vimeripotiwa barani Afrika ingawa wagonjwa waliofanyiwa vipimo wamekutwa kuwa hawana maambukizi ya virusi hivyo.
Nchini Kenya, siku ya jumanne, mwanafunzi aliwekwa karantini hospitalini katika mji mkuu Nairobi, baada ya mwanafunzi huyo kutokea katika mji wa Wuhan nchini China, eneo ambalo ndio chimbuko la mlipuko huo.
Hadi sasa virusi hivyo vimesababisha vifo 213 nchini China na maambukizi kwenye mataifa mengine 16.

