OFISI ya Taifa ya Mashtaka nchini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaro imemuunganisha katika kesi ya uhujumi uchumi wa zaidi ya shilling Bil.3, aliyekuwa Meneja wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL), Elizabeth Makwabe.
Kamanda wa TAKUKURU mkoani humo, Holle Makungu, amesema Makwabe anashtakiwa kwa makosa ya kutumia nyaraka za uongo, kughushi, wizi, pamoja utakatishaji fedha wakati akiwa mtumishi wa umma.
