TIMU ya masoko ya Kampuni ya Global Publishers, Jumamosi, Januari 1, 2020, ilimwaga fedha kwa wasomaji wao waliokutwa wanasoma Gazeti la Championi Jumamosi ambalo huchapishwa na kampuni hiyo.
Wasomaji mbalimbali waliokuwa wakisoma gazeti hilo ambalo hutoka kila siku ya Jumamosi, walirudishiwa fedha zao walizotumia kununua gazeti hilo. Promosheni hiyo ilifanyika maeneo mbalimbali jijini Dar.
Wasomaji hao walionekana kufurahia promosheni hiyo ambayo itakuwa endelevu kwa siku za Jumamosi. Wiki ijayo una nafasi ya wewe kurudishiwa fedha uliyotumia kununulia Gazeti la Championi Jumamosi linalouzwa Sh 800, kama utakutwa na Mr Championi unasoma gazeti hilo.
Na Mwandishi Wetu






