IDADI ya vifo kutokana na virusi vya corona imepanda na kufikia watu 492 nchini China, huku visa vipya kwenye meli ya abiria ya Japan kisiwani Hong Kong na maeneo mengine vikionyesha ongezeko la kusambaa kwa virusi hivyo.
Waziri wa Afya wa China Katsunobu Kato amesema watu kumi kutoka kwenye meli hiyo ya kifahari wamegundulika kuwa na virusi hivyo na kupelekwa hospitali, wakati wahudumu na abiria 3,700 wakiendelea kuwekwa chini ya karantini kwenye meli hiyo kwa siku 14.
Mjini Hong Kong, wafanyakazi wa hospitali wanafanya mgomo kudai mpaka wa kisiwa hicho na China bara ufungwe kabisa ili kuzuia virusi hivyo, lakini visa vinne vipya vilivyoropotiwa mjini humo vinaashiria kuwa ugonjwa huo unasambaa ndani ya mipaka ya kisiwa hicho.