Rais Dkt John Magufuli, leo Februari 06, amehudhuria katika mkutano wa wiki ya sheria unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar.
Aliyoyasema Rais Magufuli:-
Kuna msongamano kwenye Magereza zetu, Kuna wengi kesi zao ni za kusingiziwa au wengine wako Mahabusu kutokana na maamuzi ya bosi mmoja kusema kwamba, kwanza utakaa mahabusu.
Bado kuna changamoto ya dhulma kwa Wanawake hasa Wanawake Wajane na migogoro ya ardhi.
Sina hakika kama Mabaraza ya Ardhi yanafanya kazi vizuri pengine yapo chini ya Wizara ya Ardhi, lakini wanapoharibu lawama zinarudi kwa Mahakama.
Naipongeza Sekta ya Sheria na Mahakama nchini kwa kupata mafanikio makubwa ikiwemo kupungua kwa muda wa usikilizwaji wa kesi na kuimarisha matumizi ya TEHAMA
Matumizi ya TEHAMA yameongeza kasi ya ukusanyaji wa maduhuli kutoka Bil.1.6 kwa 2017 hadi Bil.2.6, 2019 > Pia, Mafanikio yamechangiwa na uamuzi wa Serikali kuteua Majaji 11 wa Mahakama ya Rufani, Majaji 39 Mahakama Kuu na kuajiri Mahakimu 396