MWANADADA mwenye umbo dogo kutoka Bongo Movie, Wanswekula Zacharia Lotti ‘Dorah’ amefunguka kwamba kwa kipindi kirefu amekuwa akitamani kuitwa mama lakini kikwazo ni kwamba mambo yake yalikuwa hayajakaa sawa.
Akichonga na Amani, Dorah alisema kuwa alikuwa akitafuta mtu sahihi wa kuzaa naye na pia kuweka mambo yake sawa, hivyo kwa sasa vyote hivyo vimekamilika anasubiri Mungu ampatie mtoto na anatamani awe wa kike.
“Natamani sana kuitwa mama, tena naomba Mungu anipatie mtoto wa kike nitafurahi mno, nadhani sasa ni muda sahihi wa mimi kuzaa kwa sababu nipo na mtu sahihi,” alisema.
Stori: Memorise Richard
