
Ikiwa sasa ni Takribani wiki ya tatu tangu Gazeti namba moja Tanzania la Michezo la Championi kuingia na kutoa fursa ya kuwarudishia wasomaji fedha zao walizonunulia kutoka kwa Mr. Championi wasomaji wa gazeti hilo wamefurahia ofa hiyo wakiahidi kutoa hamasa kwa wengine.
Kama kawaida kila Jumamosi Mr. Championi huingia mtaani na kuwarudishia fedha zao wanaokutea wakilisoma gazeti hilo ambapo leo Februari 08/2020 timu ya Maofisa masoko Wa Global Publishers walitembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo maeneo ya Tabata Kisukuri, Tabata Mawenzi na maeneo mengine.
Mr. Championi alikuwa akiwarudishia fedha wasomaji waliokutwa wakisoma gazeti la Championi ambapo pia hii ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuendelea kuwajali wasomaji wake.

Kwa upande wao wasomaji waliokutwa na Mr. Championi na kurudishiwa fedha zao wamefurahi na kueleza kuwa wataendelea kulinunua gazeti hilo kutokana na kuwa na habari nyingi za ukweli na zenye kuvutia ambazo wakizisoma hunufaika nazo.
Gazeti la championi huchapishwa na kampuni ya Global Publishers likihusisha Habari zote za michezo na burudani.