Mchezaji wa Rhino Rangers ya Tabora Nizar Khalfan amefiwa na mke wake (Pichani) jana Jumapili, Februari 9, 2020, mchana jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Uongozi wa Rhino Rangers imeeleza kuwa Nizar amekutwa na msiba huo akiwa na timu yake jijini Tanga ambapo alitakiwa kuwemo kwenye kikosi kilichoanza dhidi ya Sahare All Stars, katika mchezo wa Ligi daraja la Kwanza.
Nizar aliwahi kuichezea Klabu ya Yanga, Vancouver Whitecaps na Timu ya taifa ya Tanzania. Tunatoa Pole kwa Nizar Khalfan pamoja na ndugu jamaa na Marafiki.
