×

Sane anaiwahi Real Madrid

MANCHESTER, England |
KIUNGO mshambuliaji wa Manchester City, Leroy Sane, anatarajiwa kuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachopambana na Real Madrid mechi ya hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Mjerumani huyo ambaye alikuwa nje ya uwanja tangu alipoumia Agosti, mwaka jana, tayari ameanza mazoezi mepesi.

Man City na Real Madrid zinatarajiwa kucheza Februari 26, mwaka huu ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati Sane akirejea, klabu hiyo inaweza kumkosa Rahim Sterling ambaye wikiendi iliyopita aliumia.
PARIS, Ufaransa

Leave a Comment