KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Jonathan Shana, amemkanya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kuacha tabia ya kupenda kutafuta mtaji wa kisiasa katika masuala yanayohusu uchumi na uzalendo wa nchi.
Kauli hiyo imetokana na maagizo aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, Mrisho Gambo, kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuwatafuta wale wote waliosambaza picha zenye kuonyesha uharibifu wa miundombinu ya barabara katika eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Baada ya agizo hilo, Lema aliibuka na kuandika kupitia akaunti yake ya Twitter;


