×

Watoto Wafariki kwa Kujipikia Chakula Chenye Sumu

WATOTO wawili wamefariki dunia huku wengine 11 wakipelekwa hospitali baada kula vitafunwa mfano wa hamri vinavyosadikiwa kuwa na sumu nchini Uganda.

 

Watoto hao wote 13 wanatoka katika familia moja Budumba, magharibi mwa Uganda na wana umri wa kati ya miaka mitano na sita.

 

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba watoto hao walijipikia wenyewe vitafunwa hivyo mfano wa mahamri ambavyo vinafahamika kama Kabalagala na miongoni mwa viambato walivyotumia wakati wanapika ilikuwa dawa ya kuua wadudu ambayo hunyunyizwa kwenye matikiti maji na mbogamboga zinazokuzwa, wakidhani kwamba ni mafuta.

 

Leave a Comment