KIJANA Dennis Yego (24) ameishangaza Kenya baada ya kuandika maneno ya kujitakia kifo chema “Rest in peace to me” kupitia ukurasa wake wa Facebook na baadaye akaandika, ‘Kama unanidai nione kabla ya mchana wa kesho’, kabla ya kujiangamiza.
Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Februari 17, 2020, majira ya saa 2:05 usiku kabla ya Yego kumchoma visu kifuani mkewe kisha na yeye kujinyonga hadi kufa kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kifamilia.
Walter Teno ambaye ni mwenyekiti wa eneo hilo alisema kijana huyo alimfuata kwa kuwasuluhisha kwa ugomvi aliokuwa nao na mkewe.
Mwenyekiti ameshangazwa na tukio hilo kwa kuwa alidhani waliyamaliza. Alisema kijana huyo alimpiga mkewe visu vingi lakini hakufa kwa sasa yupo hospitali ya rufaa ya Kapsabet.
Kamanda wa Polisi wa kituo cha Nandi, Samson ole Kine alisema walikuta mwili wa kijana huyo ukibembea kwenye mti na kwamba hakuacha waraka wowote.
Chanzo: Daily Nation


