Bibi mmoja (pichani) ambaye majina yake hayajafahamika mara moja amezua taharuki miongoni mwa wasafiri na wananchi wengine katika Bandari ya Zanzibar baada ya watu kumfananisha na aliyekuwa Mwimbaji Nguli wa taarab, Marehemu Fatuma Binti Mbaraka maarufu kama Bi. Kidude huku baadhi wakidai kuwa ni yeye ‘amefufuka’.
Bi. Kidude aliyewahi kutamba na ngoma zake kali ikiwemo ‘Muhogo wa Jang’ombe’ alifariki dunia Aprili 17, 2013 visiwani Zanzibar baada ya kuugua maradhi ya Kisukari na matatizo ya Kongosho akiwa na umri unaokadiriwa kuwa ni miaka 102.

