YANGA imepata sare tatu za mfululizo chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Luc Eymael walizozipata walipocheza na Mbeya City, Tanzania Prisons na Polisi Tanzania.
Kikubwa kinachoikwamisha Yanga kupata sare hizo ni kutokana na kipindi cha pili kuchoka na kuishiwa na pumzi hasa kwenye safu ya kiungo inayochezwa na Papy Tshishimbi na Haruna Niyonzima na keshokutwa Jumapili itajitupa tena kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga kucheza na Coastal Union.