×

St. Mary’s Waukubali Ubora Sabuni za King Limau na Marhaba

Group Business Developer wa Azania, Joel Laizer  akizungumza na wanafunzi hao.

 

MAKAMPUNI ya Azania Group  ambao ni watengenezaji wa sabuni bora za King Limau na Marhaba ambazo zinasifika kwa ubora, wakishirikiana na kikosi cha Matangazo cha Makampuni ya Global Group, jana Ijumaa, Februari 21, 2020, walitembelea Shule ya St. Marys iliyopo Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam na kuwaonesha kwa vitendo walimu na wanafunzi ubora wa sabuni hizo.

 

Laizer (kulia) akizungumza na wanafunzi.

 

Kikosi hicho kikiongozwa na Group Business Developer (Ofisa Maendeleo ya Biashara) wa Azania, Joel Laizer kwa kuwaonyesha walimu na wanafunzi hao maajabu ya sabuni hizo jinsi zinavyoondoa madoa sugu kwenye nguo ndani ya muda mfupi.

 

Sehemu ya wanafunzi hao wakisikiliza matumizi ya sabuni hizo.

 

Pamoja na kufua na kusafishia vitu mbalimbali kama uoshaji wa magari na vyombo vingine wanafunzi hao walifundishwa jinsi ya kuosha mikono yao kupitia sabuni hizo.

 

Wanafunzi waliojipatia zawadi za sabuni za King Limau na marhaba baada ya kujibu vizuri maswali ya usafi.

 

Ilikuwa ni furaha ya aina yake kwa wanafunzi wa shule hiyo wanaoishi bwenini shuleni hapo baada ya kugundua sabuni hiyo inavyoondoa madoa sugu na kurudisha kwenye ubora wake nguo iliyofubaa.

 

Mmoja wa wanafunzi akinawa mikono na Sabuni ya Marhaba.

 

Baada ya kuoneshwa kwa vitendo sabuni hiyo inavyofanya kazi wanafunzi hao walikimbilia bwenini na kurudi na marundo ya nguo chafu na kuanza kushindana kuzifua na kuonesha mng’aro.

 

Sambamba na mng’aro wa nguo hizo wanafunzi hao walisema wamefurahishwa na harufu nzuri ya sabuni hizo.

 

Wanafunzi wakionesha jinsi ya kunawa mikono na sabuni hizo.

 

Baada ya kugundua maajabu ya sabuni hizo, wengi wa wanafunzi hao waliahidi kuwa mabalozi wa King Limau na Sabuni Marhaba kwenye familia zao na kuwaelimisha kuwa haichubui mikono kama sabuni nyingine na zina harufu nzuri.

Mwanafunzi akinawa mikono.

 

Akizungumza shuleni hapo, Laizer aliwashukuru walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa nidhamu ya hali ya juu waliyoonesha wakati wa zoezi hilo.

 

Mwanafunzi akinawa mikono.

 

Wakati zoezi hilo likiendelea wanafunzi hao walikuwa wakiulizwa maswali yaliyoendana na suala la usafi na kuonesha upeo wa hali ya juu katika kuyajibu maswali hayo.

 

Akizungumza baada ya zoezi hilo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Isaac Tamaro alisema anaishukuru sana Azania Group of Companies kuanza kutoa elimu hiyo ya usafi kwa wanafunzi wake.

Wanafunzi wakijibu maswali ya usafi.

“Hili ni somo tosha, ambalo naamini wanafunzi wangu wamenufaika nalo vyakutosha maana usafi ni sehemu ya maisha ndiyo maana kila mtu anapenda kuonekana msafi”. Alimaliza kusema Mwalimu Tamaro.

 

Naye Mkurugenzi wa Shule hiyo, Rose Rwakatare alitoa shukrani kwa Azania Group of Companies kuichagua shule yake na kwenda kutoa elimu ya usafi pamoja na kuwaonesha jinsi sabuni hizo zinavyofanyakazi.

Wanafunzi wakifua kwa sabuni za King Limau na Marhaba ambazo hazichubui mikono kama sabuni zingine na kufurahia harufu yake nzuri.

 

Mkurugenzi Rose aliikaribisha kampuni hiyo kwenda kutoa elimu kwenye shule zake zingine zilizopo sehemu mbalimbali ikiwemo, Tabata, Mbagala na kwingineko ikiwemo mikoani.

 

Kampuni hiyo sambamba na kutengeneza sabuni hizo sasa inazalisha unga wa ngano wenye ubora wa hali ya juu ambao haupatikani sehemu nyingine yeyote pamoja na mafuta ya kupikia yanayotengenezwa kwa ufanisi wa hali ya juu.

Group Business Developer, Joel Laizer (kushoto) akimkabidhi zawadi ya sabuni, Mkurugenzi wa shule za St. Marys, Rose Rwakatare kwa niaba ya wanafunzi baada ya kumalizika zoezi hilo.

Akiyazungumzia mafuta hayo Joel alisema kabla ya kufika kwa mtumiaji yanachujwa mara tatu na mitambo kutoka Bara la Ulaya na hivyo kuwa na viwango vya Ulaya.

 

Joel amesema bidhaa hizo ambapo ni mkombozi kwa wananchi mbalimbali wakiwemo mama lishe, wafanyakazi wengine tayari zinapatikana nchi nzima kwenye maduka mbalimbali ya mitaani, Supermarket na kwingineko.

HABARI:NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

Leave a Comment