×

VIDEO: WAZIRI MKUU Aanika Serikali Ilivyothibiti Wizi wa Madini

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo Jumapili Feburuari 23, 2020 anazindua Hati ya uhalisia ya madini kwa Tanzania ambayo itatumika kutambulisha aina ya madini ya bati yanayozalishwa nchini.

Hati hii kwa Tanzania inakuwa ni hati ya kwanza ambayo inatibitisha umiliki wa madini na haikuwahi kuwepo nchini kutokana na sheria za nyuma za madini kutokikidhi vigezo vya ubora wa kikanda.

Akihutubia katika Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka 2020 uliobeba kauli mbiu ya “Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya madini” umehudhuriwa na mawaziri wa madini kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Uganda na Congo ameyasema haya:_

“Wizara ya Madini ihakikishe mkutano huu unaendelea kuimarishwa ili uwe na mchango katika sekta hiyo muhimu”

“Katika kukabiliana na utoroshwaji wa madini, tuliamua kuanzisha masoko ya madini, hadi sasa tuna maduka ya masoko ya madini 27 katika mikoa yote na vituo vidogo vya ununuzi wa madini 28”

Kwa upande wa Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amesema haya katika mkutano huo;-

“Leo hii Watanzania wananunua, wanafunga na kuuza madini katika masoko ya kimataifa tofauti na ilivyokuwa hapo awali, wachimbaji wanamshukuru sana Rais Magufuli kwa fursa hii iliyowapa heshima”

“Kama kuna jambo jema limetokea katika sekta ya madini basi tumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa maono yake ya kuleta mapinduzi katika sekta hii muhimu kwa uchumi wa nchi yetu”-Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko

“Sekta ya madini imeendelea kuimarika na mchango wake umeendelea kukua kutoka asilimia 3.1 mwaka 2015 na sasa ni 5.1 ukilingalisha na kule tulikotoka, pia sekta ya madini ni ya pili kwa ukuaji ikifuatia wizara ya ujenzi”

Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka 2020 uliobeba kauli mbiu ya “Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya madini” umehudhuriwa na mawaziri wa madini kutoka nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Uganda na Congo na unafungwa leo na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Leave a Comment