×

Yanga Ndio Nini….

LICHA ya kuanza na mastaa wazawa sita ambao wanaweza kukipiga kwenye viwanja vya mkoani bado haikuwa msaada kwa Yanga jana kuchukua pointi mbele ya Coastal Union.

 

Kikosi hicho kwa mara nyingine kilikwama kupata pointi tatu kwenye mechi yake ya nne mfululizo katika Ligi Kuu Bara baada ya kwenda suluhu na Coastal wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

 

Yanga kwa asilimia kubwa walibadilika kwa kuanza na sura za wazawa lakini bado walikwama kuzitikisa nyavu za Coastal ambao walibana vilivyo mastaa hao wa Yanga.

 

Hii ni mechi ya nne mfululizo Yanga katika ligi wanakwenda sare na kuifanya kufikisha pointi 41 wakiwa nyuma ya vinara Simba kwa pointi 21.

 

Mechi nyingine za ligi ambazo Yanga walipata sare mfululizo ni pamoja na Mbeya City 1-1, Prisons 0-0 na Polisi Tanzania 1-1.

 

Katika mechi hiyo kipa wa Yanga, Metacha Mnata alikuwa shujaa baada ya kuokoa hatari zaidi ya tatu katika kipindi cha pili ambapo Coastal walikuwa moto kutokana na kucheza soka la kushambulia kwa sana.

 

Yanga kwenye mechi hiyo hawakuwa na madhara makubwa kwa wapinzani wao katika kipindi cha kwanza ambapo hawakuwa na shuti ambalo lililenga lango la Coasta Union.

 

Kikosi cha Yanga kilichoanza ni Metacha, Juma Abdul, Jafari Mohamed, Lamine Moro, Said Makapu, Papy Tshishimbi, Haruna Niyonzima/Eric Kabamba, Balama Mapinduzi/Mrisho Ngassa, Bernard Morrison, Ditram Nchimbi, Seif Tariq/ Ally Sonso.

 

Wachezaji wa kimataifa ambao walipumzishwa katika mechi hiyo ni Farouk Shikalo, David Molinga, Patrick Sibomana na Yikpe Gislein.

 

Kikosi cha Coastal; Sudi Abdallah, Hassan Kibailo, Hans Masudi, Ibrahim Ame, Bakari Mwamnyeto, Salum Ally, Mtenje Albano, Ayoub Semtawa, Mudathir Said/Hija Ugando, Ayoub Lyanga na Issa Said.

 

Karibu vigogo wote wa Yanga walikuwa jukwaani wakionekana ni wenye huzuni kubwa na baada ya mchezo ziliibuka vurugu za baadhi ya mashabiki dhidi ya baadhi ya vigogo jukwaani. kutocheza kwa kipindi kirefu tofauti na mwenzake ambaye ametoka kwenye timu yake akiwa bado anacheza kwenye kiwango kizuri.

Leave a Comment