×

Waafrika Waishio Wuhan Kurejeshwa Nyumbani

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameagiza kuondolewa kwa raia wa nchi hiyo waishio katika Jimbo la Wuhan nchini China kutokana na mlipuko wa Coronavirus.

 

Raia 132 kati ya 199 waishio Wuhan wamesema wanataka kurudi nyumbani. Serikali imeamua kuwa wakifika watawekwa eneo maalumu kwa siku 21.

 

Hadi sasa watu 2,800 wamefariki kutokana na ugonjwa huo huku 83,000 wakiripotiwa kupata maambukizi ya virus vya Corona.

 

Leave a Comment