×

Mbelgiji Yanga SC Apangua Kikosi

 

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Mbelgiji Luc Eymael, ameshtuka na kupitisha maamuzi ya kupangua kikosi chake kuelekea mchezo mkali dhidi ya Simba, Jumapili hii.

 

Mbelgiji huyo amefi kia maamuzi hayo, baada ya kuona kuna uwezekano wa mastaa wake ambao ataanza nao kwenye mechi hiyo na Simba kupata kadi au majeruhi ambayo yanaweza kufanya wakaikosa mechi hiyo itakayopigwa Machi 8, katika Uwanja wa Taifa.

 

Kocha huyo amefi kia maamuzi ya kuwapumzisha nyota wake kadhaa kwenye mechi yao ya kesho Jumanne dhidi ya Mbao ambapo miongoni mwa watu ambao hawatakuwepo ni kipa aliye kwenye kiwango cha juu kikosini hapo, Metacha Mnata.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mbelgiji huyo amesema kuwa atawapumzisha nyota wake kadhaa akiwemo Metacha kwa ajili ya kuwapisha wengine wacheze kuepuka majeraha.

 

“Kumekuwa na wimbi la majeruhi kwa siku za karibuni kwa hiyo kuna njia ya kuepuka na kufanya mabadiliko katika kikosi.

“Kwenye mechi yetu na Mbao nitawampumzisha wachezaji kadhaa akiwemo Metacha na kuwachezesha wengine.

 

“Kwenye mechi hiyo wachezaji kama Papy Tshishimbi, Ditram Nchimbi wataanza lakini hawatacheza kwa dakika zote 90, nitafanya mabadiliko kwao kwa kuepuka majeruhi katika mechi zetu zijazo,” aliweka nukta Mbelgiji huyo.

 

SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave a Comment